SEMINA YA NENO LA MUNGU
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWL MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI
Kusoma sehemu iliyopita Bonyeza Hapa
Sehemu ya 5
Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.
28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?
Jana tuliangalia mamlaka zizizomo ndani ya mwali leo twende ndani kidogo kuendelea na somo hili
Mwanzo 1:26-27 ‘’ 26Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.’’27Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba.
Hapa tunaona Roho ya mwanadamu ikiumbwa na ikipewa mamlaka yote na Mungu ya kwenda kutawala viumbe vyote vya baharini na ndege wa angani na kila kiumbe. Lakini utekelezaji wake iliatakiwa utokee katika Mwili.
Mwanadamu aliumbwa na 1. Sura ya Mungu.
2.Mfano wa Mungu
3.Alipewa na ufalme wa Mungu
4.Alipewa na mamlaka ya kutawala.
2Wakorintho 5:15 kufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. 15Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi WASIISHI TENA KWA AJILI YA NAFSI ZAO WENYEWE, BALI KWA AJILI YAKE YEYE ALIYEKUFA NA KUFUFUKA TENA KWA AJILI YAO.
Hivyo hapa duniani tulipopewa mwili ni kwa ajili ya kufanya kusudi la Mungu na sio kufanya mapenzi yetu. Kwa hiyo hatuishi tena kwa ajili yetu bali tunaishi kwa ajili ya Mungu. Huu mwili tulio nao haoa duniani ni kwa ajili ya kufanya mapenzi ya Mungu. Maana mwanadamu ni roho.
Warumi 14:7-8 ‘’ 7Kwa kuwa hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna hata mmoja wetu afaye kwa ajili yake mwenyewe. 8Kama tunaishi, tunaishi kwa Bwana, nasi pia tukifa twafa kwa Bwana. Kwa hiyo basi, kama tukiishi au kama tukifa, sisi ni mali ya Bwana
Umeona huo mstari yaani hakuna mtu anayeishi hapa duniani kwa ajili yake mwenyewe ina maana waote tunaishi hapa duniani ili tuyafanye mapenzi ya Mungu. Hili ni jambo la muhimu sana na ndio maana kuna siku ya kutoa hesabu namna ulivyofanya kazi ya Mungu hapa duniani.
Kwa hiyo Roho ya Mwanadamu haijapewa umiliki wa mwili yaani imepewa uangalizi tu wa kuutunza mwili kwa ajili ya kufanya yale mapenzi ya Mungu.
TWENDE TUANGALIE MFANO WA NDOA.
1Wakorintho 7:14 ‘‘4Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.’’
Umeona hapo yaani Mamlaka ya mwili wa mwanaume anayo mke wake na mamlaka juu ya mwili wa mwanamke anayo mume. Kwa hiyo mwili wa mwanaume ni kwa ajili ya mke wake na mwili wa mwanamke ni kwa ajili ya mume wake. Kama ni hivyo sasa roho ya mwanamke hukaa kwa kwenye wili wa mwanaume na hivyo hivyo kwa mwanaume. Ndio maana Mungu alisema hawa si wawili tena bali wamekuwa mwili mmoja. Sasa biblia inasema pasipo roho mwili umekufa na kufa maana yake ni kukosa mawasiliano. Kwa hiyo katika ndoa mkikosa mawasiliano ina maana ndoa inakuwa inakufa maana yake kunakuwa hakuna kuzaa. Kwa hiyo kama mtaendelea kutokuwa na mawasiano vizuri ina maana ufa unatokea na msiposhughukia vizuri ndoa inakufa kabisa. Kinachokata umiliki ndani ya ndoa ni roho ya mauti maana biblia inasema mishahara wa dhambi ni mauti.Kwa hiyo roho zisipopata nafasi halali ndani ya ndoa ina maana mawasiano baina ya mke na mume yatakufa na kufanya ndoa kufa kabisa. Sasa siko kwenye somo la ndoa twende twenye sehemu nyingine.
POINT YA 6: ILI MAMLAKA YA ROHO IWEZE KUTUMIKA DUNIANI NI LAZIMA MWILI UTUNZWE NA ROHO HIYO.
Mwanzo 1:28 Tunaona Adam aliumbwa na akiwa na
i): Akiwa roho
ii): Alipewa kuzaa
iii): Kuongezeka
iv):kuijaza nchi.
Mungu alipozungumza nae kwa ajili ya kuzaa akiwa katika roho alikuwa anataka matokeo ya mambo hayo yaonekane katika ulimwengu wa kimwili.
Ndio maana Yesu alipewa mwili ili aweze kutembea kwenye mamlaka. Ndio maana biblia inatuambia kanisa ni mwili wa kristo na Yesu ni kichwa cha kanisa. Hivyo mwili bila kichwa hauwezi kufanya lolote. Ili kanisa lijue namna ya kutembea kwenye mamlaka inatupasa tujue namna ya kuishi ndani ya Kristo hapo ndipo tutaweza kutembea kwenye mamlaka.
Kwa iyo unapookoka unakuwa kiungo katika mwili wa Kristo. Kwa hiyo Yesu akitaka kuhubiri anaingia ndani ya mtu na ndipo anakwenda kuhubiri na Yesu hawezi kufanya chochote pasipo watu wake kuchukua hatua. Hii yote ni sheria iliyopo kwenye ulimwengu wa roho na huu wa damu na nyama. Na ni mwamdamu tu peke yake ndie kapewa mamlaka hizi mbili ndani ya mwili na katika ulimwengu wa roho. Mungu hana na wala malaika hawana. Hii ni heshima kubwa sana ambayo mwandamu kapewa na Mungu. Laiti kila mmoja akielewa sana upana wa mambo haya atakuwa amepata kitu kikubwa sana.
ANGALIA SASA UUUMBAJI WA MWILI WA MTU.
Anzia Luka 1:30-35 ‘’ 30Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.”
34Maria akamwuliza huyo malaika, “Maadam mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?”
35Malaika akamjibu, “ROHO MTAKATIFU ATAKUJILIA JUU YAKO, NAZO NGUVU ZAKE YEYE ALIYE JUU ZITAKUFUNIKA KAMA KIVULI, KWA HIYO MTOTO ATAKAYEZALIWA ATAKUWA MTAKATIFU, naye ataitwa Mwana wa Mungu.
Malaika Gabriel alimwambia kuwa kile kitakachozaliwa kitakuwa kitakatifu. Kwa hiyo mwili wa mwanadamu unakuwa na vitu 3.
i): Udongo
ii): Neno
iii): Roho mtakatifu.
Sasa tukirudi kwenye kitabu cha Mwanzo1 & 2 tunaona hapo Mwanzo Mungu akiumba mbingu na nchi. Na sura ya pili tunaona Roho mtakatifu akitulia juu ya maji na Sura ya tatu tunaona Mungu akisema .
Kuanzia pale kila kitu kilikuwa kinaumbwa na Roho mtakatifu na kilikuwa na Roho mtakatifu. Ila ilipofika kutengeneza mwili Mungu aliifanya mwenyewe.
Akachukua udongo akaumba mwili na akupulizia pumzi na mwamadamu akawa nafsi hai.
POINT YA 7: MWILI ULIPOUMBWA ULIKUWA NA UHAI WA AINA MBILI.
Yakobo 2:26 ‘’ 26Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa. Mwili pasipo roho umekufa. Hivyo mwili wa Adamu ulibeba roho mbili.
i): Roho Mtakatifu
ii): Ilibeba roho wa mtu.
Roho zote hizi mbili zilikaa ndani ya mtu na zote zilikuwa hai.Kwa hiyo hata mwili kufa unatakiwa ufe vifo viwili. Adamu alipokorofisha, Mungu alimwambia hakika utakufa. Ona matokeo yake alipokaa kikao na Mungu. Baada ya mazungumzo na Mungu tunaona Adam na mke wake akifukuzwa kwenye bustani ya Edeni.
Roho ile ya kutoka kwa Mungu iliyokuwa ndani yake kwa Adamu iliondoka. Na Adam akabaki kama alivyo.
1: Hana neno la Mungu ndani
2: Hana ufalme wa Mungu
3: Hana Sura ya Mungu.
4: Hana mfano wa Mungu.
Na baadae tunaona Mungu akimpa adhabu Adamu. Na hapa ndipo kifo cha pili kilitokea.Angalia Mwanzo 3:19 b ‘’ kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.’’. hapa tunaona kifo cha pili cha Adamu.
Rumi 5:12 ‘’ 12Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi.
Biblia inatuambia dhambi ni uasi na uasi maana yake ni kwenda kinyume cha mamalaka ambayo umepewa au auko chini yake.Kuingia kwa dhambi duniani kuliua roho ya mtu , kuvuruga nafsi na kuua mwili wa mtu.na sheria ya Dhambi na mauti ikaanza kutawala.
TUANGALIE MFANO WA YESU.
Yesu alipewa nae mwili na ndio maana Mariam aliambia kuwa Roho atakujia ina maana Roho Mtakatifu na NENO ndio mbegu iliyomleta Yesu. Hivyo kuja kw nguvu za Mungu na kumfunika Mariam na tunaona hapo Roho na neno kuchnganyikana na kuunda mwili wa Yesu.
Kifo cha Yesu kilikuwa kwa aina mbili.
Alipokuwa msalabani alisema Eloi Eloi lama saba ki tani, Ina maana Roho wa Mungu alimtoka na akabaki na mwili ili aweze kulipa gharama ya na adhabu ya dhambi akiwa hai. Hiki ndicho msumbua sana Yesu hata pale getsemane maana alikuwa hajui kabisa kukaa mbali na baba yake.
Baada ya hapo tunaona ya kuwa Yesu alisema naona kiu, yaani hakuwa anahitaji uwepo wa baba yake . Haikuwa kiu ya kawaida bali ilikuwa ni ie hali ya kule ndani ya kutafuta uwepo wa baba Yake maana ullikuwa tayari umepotea. Na unaona mwisho akipaza sauti yake akiitwaa roho yake.
POINT YA 8 KIFO CHA KWANZA CHA MWILI NDICHO KILICHOMNYANG’ANYA MWANADAMU MAMLAKA YA KIROHO YA KUTAWALA HAPA DUNIANI.
Warumi 5: 12-14 ‘’ 12Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi. 13Kwa maana kabla sheria haijatolewa, dhambi ilikuwepo ulimwenguni. Lakini dhambi haihesabiwi wakati hakuna sheria. 14Hata hivyo, tangu wakati wa Adamu hadi wakati wa Mose, mauti ilitawala watu wote hata wale ambao hawakuvunja amri kama alivyofanya Adamu, ambaye alikuwa mfano wa yule atakayekuja
Kabla ya sheria ina maana ilikuwepo na ilipata nafasi baada ya Adamu kuifungulia mlango. Na hiki kifo cha kwanza ndicho kilichonyang’anya mamlaka ya kiroho ya mwandamu. Na ndio maana Mungu alikuwa hamuoni kwenye mamlaka yake aliyokuwa nayo na hapo ndipo alipomuuuliza Adamu uko wapi.
Mwanadamu peke yake ndiye aliyewekwa na Mungu ili atawale kote kote kweye ulimwengu wa roho na ulimwengu wa Mwili.
Mungu hawali mambo yote haya ya ulimwengu wa mwili maana haya yalikuwa ya mwandamu. Ila alipoasi hapa duniani ndicho kilichomponza mwanadamu. Na akakosa neno la ufalme maana mfalme hutawala kwa neno. Neno la Mfalme ni final. Na ukiasi unafungwa ila mwandamu akapoteza yote haya. Ndio maana sasa unaona ajali zinatokea hapa duniani na unahisi ni Mungu, sio kweli Mungu hasababishi ajari hizi tunazoziona.
Matokeo tuanyoyaona hapa duniani ni matokeo ya uasi wa mwanadamu kwa hiyo yuko chini ya sheria ya dhambi na mauti. Na ndio maana tunaona mauti inawatawala. Na shetani kujua hili ndio maana akatengeneza ufalme wake ambao sasa uko chini ya sheria hii ya dhambi na mauti.
Mungu anapokupa neema ya kurudi kwake anakurejeshea tena ile nafasi ambayo ilipotea pale bustani ya Edeni.
POINT YA 8. YESU ALIUTOA MWILI WAKE UWE SADAKA ILI KUTUPA MBINU ZA KUTUSAIDIA ILI MWILI UWE UPANDE WA MUNGU.
Ili tuishi hapa duniani ni lazima tumzalie Mungu matunda. Ukisoma Warumi 8:1-11 utaona Mungu akituwekea torati ndani yetu, yaani sheria zake katika moyo wetu na huvyo basi hata kama tuko kwenye kipindi cha neema bado torati inafanya kazi. Kama mtu ulikufa mara mbili lazima ufufuliwe mara mbili. Yaani uokoke au uzaliwe mara ya pili ili kufufua roho yako na unahuishwa mwili wako na nafsi yako inabdilishwa na kufanywa upya ili uweze kutembea hapa duniani katika uweza na mamlaka ambayo Mungu amekupa.
Unakuwa umefufuliwa na umeketishwa pamoja na kristo na Yesu anakuwa anaishi ndani yako na ufalme na enzi vyote vinakurudia tena kama vile Mungu alivyokuwa amekusudia mwanadamu awe. Ooh hii ni sri ya ajabu unahitaji kujua… haleluya haleluya.
Wana wa Israel japo walipita jangwani lakini bado hata miili yao haikuchakaa hata miguu yao haikuchakaa. Na wakati ule Roho mtakatifu alilikuwa nje yaani akiwafunika kwa wingu. Je si Zaidi sana sasa maana Roho mtakatifu yupo ndani yetu yaani anafanya kazi kutokea ndani yetu. Na ukijua hii siri utaona kabisa Mungu anaushikilia mwili wako japo umri unaenda ila unakuwa hauzeeki.
Biblia inatuambia kuwa wana wa Israel hawakuingia ile nchi ya ahadi kwa sababu ya kutokuamini kwao yaani neno la Mungu hakichanganyikana na Imani. Ambayo Imani inageuka kuwa chakula cha roho ambacho ndicho kinafanya Baraka maishani mwako.
MFANO WA PETRO.
Mwaka mmoja nilipokuwa Israel katika ziwa Galilaya nikiwa najiuliza ile hali Petro alikuwa nayo ya kutembea juu ya maji na baadae akazama. Na kilichonifanya nijiuilize sana swali ni kuwa sioni mahali ambapo maji yaligeuka sakafu na petro akapita juu yake maana hata ukiona mawimbi yalikuwepo. Na hili swali najiuliza sana kuwa je alifanyaje sana hadi aliweza kutembea juu ya maji. Wengine watasema mbona Petro alizama kwa sababu hakuwa na Imani basi nakuambia na wewe nenda kajaribu. Maana kwenye biblia tunoana Yesu akitembea juu ya maji na Petro alipomfuata alitembea na alioanza kuona mawimbi na upepo hofu ikamwingia na akaanza kuzama. Ona Yesua alichosema alisema ewe mwenye Imani haba kwanini ulliona shaka moyoni mwako. Na baadae tunoana Yesu akimwokoa Petro na kuanza kutembea nae juu ya maji na kwenda kwenye Boti.
Sasa swali langu najiuiza kwanini petro alizama. Kama ni neno alikuwa nalo na Imani alikuwa nayo sasa kwanini alizama? Kwa hiyo ili uweze kutembea kwenye mamlaka hii lazima ujue kuunganisha Imani yako na neno la Mungu na uweza wake ili uweze kutembea kwenye mamlaka. Hapo ndipo utajua kuwa muujiza wa Petro kutembea kwenye maji muujiza ulikuwa kwenye miguu yake.
POINT YA 9: NI MAMBO YAPI YANAYOFANYA MTU ALIYEOKOKA MWENYE YESU NDANI ASITEMBEE NDANI YA MAMLAKA.
Kilicho wazuia wana wa Israel ni ile habari ya wapelelezi na ikawakosesha Imani kwao nao wakashindwa kumwamini Mungu nao wakashindwa kuingia nchi ya ahadi.
Pia wanafunzi japo walipewa mamlaka ya kutoa pepo ukisoma katika Luka 9:1 Utaona pale ila bado walishindwa kutuoa pepo. Yesu aliwaambia kuwa enyi wenye Imani haba, kumbe tatizo kubwa lilikuwa kwenye Imani yao. Na aliwambia haya hayafanyiki ila kwa kufunga na kuomba, maana yake nini Imani kama haina nguvu ya Mungu haiwezi fanya kitu na ndio maana Yakobo anasema Imani bila matendo haizai..
Na ile kuwa umepewa mamlaka lazimaujue sheria, japo unapewa na Malaika na Roho mtakatifu lakini usipojua sheria zinanzotawala bado kwako itakuwa ni ngumu sana kutembea ndani ya mamlaka ambayo Mungu ametupa.
Na ukitaka malaika wakae upande wako inabid sana ujue namna ya kutii neno la Mungu ambalo ndilo linakuja na pumzi ya Mungu na Nguvu ya Mungu na ndilo linaumba Imani yako maana Imani huja kwa kusikia neno la kristo.
VIPENGELE 6 VINAYOFANYA MTU ASITEMBEE NDANI YA MAMLAKA.
1):KUTOKUKUA KIROHO.
1Wakorintho 3:1-4 Niliongea na nyie kama watoto wachanga kwa sababu mmoja anasema mimi ni wa kefa(Petro) mwingine anasema mimi ni wa Paulo na Mwingine anasema mimi ni wa Apolo. Na ona matokeo yake ya watu kutokuangalia ambacho Mungu anataka kufanya bali mnaanza kuuliza mimi unasali wapi wewe na kuweka madhehebu mbele badala ya Mungu.
Galatia 4:1-3, anasema mwana ajapokuwa mrithi lakini kama ni mdogo bado atabaki kuwa kama mtumwa hadi muda ambao baba ataamua. Kwa hiyo huwezi pewa mamlaka kama haukui kiroho.
2): KUTEKELEZA MAPOKEO YA WANADAMU NA KUFIKIRI NI NENO LA MUNGU.
Mathayo 15;6-9 Yesu alipokuwa anawaambia mafarisayo kuwa wameshikilia sana mapokeo badala ya neno la Mungu. Na waliweka mapokeo mbele kuliko kweli ya neno la Mungu.
3): WATU WALIOKOKA KUSHINDWA KUTOA MIILI YAO KAMA SADAKA.
Rumi 12:1-2 ‘’ Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema Zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
2Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuze kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni Pake na ukamilifu.
Nia ya Mwili ni kupingana na Mungu. Mwili hauendi mbinguni unaishia hapa hapa kwa hiyo mkiwa hapa duniani kama watu mliokoka unawapasa sana kuomba maombi ya kuukabidhi mwili kwa Mungu yaani uwe kama umekufa ili uweze kuishi kadri Mungu anavyopenda.
Ukitaka Mungu akutumie sawa sawa na neno lake basi jifunze sana kuutoa mwili wako uwe dhabihu kwa Mungu. Maana mwili sio wa kwako wewe ni mwangalizi.
4:JIFUNZE KUUAMBIA MOYO WAKO AU KUUFANYA AU KUOMBEA MOYO WAKO UWE TIFU TIFU ILI MUNGU ASEME NA WEWE.
Maana wapo watu waliokoka lakini wana kiburi na jeuri. Hivyo omba sana maombi haya ninayokuambia.

Comments
Post a Comment