KUHUSU VIDEO YA MWANA NA KIMASOMASO ZA ALIKIBA,SOMA HAPA...

Najua radio sasa hivi zina single mpya mbili za staa wa longtime kwenye bongofleva Ali Kiba ambae amerudi kwenye headlines baada ya ukimya wa muda mrefu.

Kama hukumbuki, mara ya mwisho Ali Kiba kutoa single kwenye radio ilikua June 2012 ambapo moja unaitwa Kimasomaso na nyingine inaitwa Mwana.

Ali ambae ni baba wa watoto watatu, anatarajia kuanza kushoot video za hizi nyimbo mbili mwanzoni mwa August 2014.


Meneja wake amesema video hizi zitafanywa na madirector wa Tanzania na kwamba sasa wanafanyia kazi jinsi zinavyotakiwa kuwa na watazifanya katika maeneo tofautitofauti.

Video zote hizo mbili zinatarajiwa kuachiwa mwishoni mwa August.

Comments