Mapema leo wamekwenda kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kukabidhi barua yenye malalamiko mbali mbali juu ya walichokisema kuwa uvunjifu wa katiba unaofanywa kwa makusudi na viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dk. Wilbroad Slaa.
Ingawa walifanikiwa kuzifikisha barua hizo sehemu zote mbili licha ya kikwazo ambacho kiliwekwa na jeshi la polisi kwenye ofisi ya mkaguzi wa mahesabu ya serikali baada ya kuonekana wamepeleka barua hizo kwa maandamo na mabango.
Chini ya hizi picha nimeambatanisha barua zote nilizopata nimeona nikuwekee na wewe usome.
Hii ni barua iliyopelekwa kwa CAG
JORUM ABDALLAH MBOGO
S.L.P 1110
TABORA
25.06.2014
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALIMTAA WA SAMORA NA OHIO
S.L.P 9080
DAR ES SALAAM
+255(22)2115157/8
DAR ES SALAAM.
YAH: MAOMBI YA TAARIFA YA UKAGUZI WA CHADEMA.
Husika na somo hapo juu.
Mimi ni mwanachama na kiongozi wa ngazi ya wilaya wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la chama
Kwa kipindi kirefu ndani ya chama chetu tumekuwa tukilalamikia matumizi mabaya ya pesa hasa za ruzuku, pesa ambazo msingi wake ni kodi za wananchi na hivyo kuwa ni pesa za umma. Hii inatokana na ukweli kwamba mpaka sasa chama kimepokea jumla ya BILION 10.038 kama ruzuku kutoka serikali kuu, kwa kipindi cha miezi 42 kutokea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Tumejitahidi sana kudai taarifa sahihi za matumizi ya pesa hizo bila mafanikio.
Kwa kuwa tunatambua kwamba ni hivi karibuni tu, ofisi yako imemaliza kufanya UKAGUZI MAALUM WA MAHESABU KWA VYAMA VYA SIASA kikiwemo na CHADEMA, na kwamba taarifa yake mmeshaiwasilisha Bungeni.
Kutokana na ukweli kwamba wengi wetu sisi sio wabunge na hatuna uwezo wa kuipata hiyo Taarifa ambayo ni muhimu sana.
Na kwa kuzingatia kwamba sisi ndio wenye chama na sisi ndio walipa kodi zinazoipatia chama Ruzuku. Ni wajibu wetu kusimamia matumizi yake.
Hivyo basi, kwa niaba ya viongozi na wanachama wenzangu wasiopungua 82, tunaiomba ofisi yako itusaidie yafuatayo
- ITUPATIE NAKALA YA TAARIFA ILIYOKAGULIWA
- IITOE NAKALA HIYO KWA UMMA ILI UMMA UJUE NAMNA KODI ZAO ZINAVYOTUMIWA
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
Wako katika ujenzi wa Taifa
……………………………………………………
JORUM ABDALLAH MBOGO
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Hii ni barua iliyopelekwa kwa msajiri wa vyama vya siasa.
JORUM ABDALLAH MBOGO
S.L.P 1110
TABORA
25.06.2014
MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASAS.L.P 63010
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Ndugu,
YAH: MAOMBI YA UFAFANUZI WA KIKATIBA JUU YA UVUNJIFU WA KATIBA NA YA CHAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI
Mheshimwa Msajiri, Somo hapo juu la husika.
Mimi ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,
Kwa niaba ya wanachama wenzangu, tunaleta kwako malalamiko ya uvunjifu wa katiba ya chama Yanayotokana na matamko yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kitaifa juu ya kuungana na UKAWA yenye tafsiri kwamba wataachiana majimbo ya kugombea ili waweze kuingia madarakani na kuunda serikali ya pamoja.
kama hivyo ndivyo wanakiuka SURA YA TISA. IBARA YA 9.3.1 ya KATIBA YA CHADEMA inayosema ‘’chama kinaweza kuunda mseto na chama au vyama vingine vyenye madhumuni na malengo yanayofannaili kuimarisha iwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au wa serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja’’
Kwa kuwa viongozi wa CHADEMA na CUF na NCCR wameungana na kuunda chama kingine cha UKAWA kwa mujibu wa SURA YA TISA ibara ya 9.3.3 ‘’chama kinaweza kuungana na chama ama vyama vingine kuunda chama kipya’’ hivyo wamevunja SURA TISA, Ibara ya 9.3.4 inayosema ‘’Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1, na 9.3.3 utafanywa na mkutano mkuu wa Taifa na kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza KUU’’.
Na hivyo sisi kama chama hatujakaa BARAZA KUU ili kupitisha AGENDA za huo mkutano mkuu na wala MKUTANO mkuu haujaitishwa kujadili maamuzi hayo yaliyofikiwa na viongozi wetu.
Mheshimiwa Msajiri, Tunafahamu kwamba KANUNI za chama SURA YA TISA kuanzia ibara ya 9.0 Mpaka ibara ya 9.7 zinatoa uhuru wa chama kuungana na kufanya ushirika na vyama vingine kwa kadri itakavyoona inafaa.
Ila kanuni hizi zinaweka mkanganyiko wa kitafsiri, na hivyo zinazuiwa na kuuliwa nguvu na Ibara ya 9.2.3 ya KATIBA YA CHAMA Inayosema ‘’kukitokea migongano kati ya kipengele cha katiba na kile cha kanuni, kipengele cha katiba kitatawala’’. Hivyo kanuni zinazotoa uhuru huo haziwezi kutumika hapa.
Mheshimiwa msajiri, kwa kuwa wewe ndio mlezi na msimamizi wa vyama vyote vya siasa, na kwa kuwa hakuna chama cha siasa kilicho juu ya katiba yake, hivyo tunakuomba uingilie kati mgogoro huu wa uvunjifu wa katiba unaofanywa kwa makusudi na viongozi wa chama.
Tunakuomba pia uuagize uongozi wa kitaifa uitishe haraka kikao cha baraza kuu, kwani tumeshapitisha miezi mi nne sasa ya kisheria ambayo baraza kuu lilipaswa kukaliwa, mara ya mwisho tulikaa kikao cha baraza kuu mwezi febryary mwaka 2013, hivyo tulitakiwa tena tukae baraza kuu mwezi February mwaka huu. Hatujaitwa, wala hatujapewa sababu yoyote yenye mantiki.
Vile vile tunakuomba uwaagize viongozi wa chama waitishe chaguzi halali za zhama na waache kuchomeka watu wao wanaowataka kwa hila, kwa mujibu wa ratiba tulizozipitisha uchaguzi ulupiswa kuwa umeshafanyika kufikia December 2013, na baadae june 2014, lakini mpaka tunavyokuandikia leo, hakuna lililofanyika.
Tunakutakia kila la heri katika kutusaidia ufafanuzi huu.
Tunatanguliza shukrani za dhati na tukiamini swala letu litafanyiwa linavyostahili.
Wako katika ujenzi wa Taifa.
JORUM ABDALLAH MBOGO
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.SOURCE;MILLARDAYO
Comments
Post a Comment