Wakali wa Tanzania walio kwenye Top 5 ya wanamuziki wa Tanzania wanaolipwa fedha nyingi kwenye show, Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz, weekend hii wametumbuiza kwenye nchi za mabara mawili tofauti.
Ommy Dimpoz na timu yake ya Pozi Kwa Pozi aka PKP walikinukisha jijini Washington DC.
“It was so memorable night in Washington DC…..Texas see yaah,” aliandika Ommy kwenye Instagram.
Ommy pia alishare picha ya noti kibao za dola alizotuzwa na mashabiki. “Hey can somebody call line 911???Dis teampozkwapoz want to kill me yooo….#thankful,” aliandika.
Kwa upande wake Diamond Platnumz na timu yake ya Wasafi aka WCB alikuwa jijini Kuala Lumpur nchi Malaysia na kufanikiwa kuvuta crowd ya kutosha pia.
“Ooooh Malaysians… you Guys Made Me cry For de Love,” aliandika Diamond.
Comments
Post a Comment