Latipher Mkuu,Silaha nyingine ndani ya World of Benefit

Jina lake halisi ni Latipher Mkuu, si maarufu sana machoni pa watu lakini ni mahiri sana katika kazi, kama ulivyo mvuto wa umbile lake ndivyo alivyo na mvuto katika kazi ya sanaa ya uigizaji. Kipaji chake kimedhihirika hivi karibuni baada ya kupata fursa ya kushiriki katika filamu ya Worl Of Benefit ambayo ipo katika hatua ya ‘editing’ ikisubiri kuingizwa sokoni.

Licha ya ushiriki wake wa ‘scene’ chache ndani ya filamu hiyo lakini Latipher ameweza kuonesha kipaji cha hali ya juu akiwa sambamaba na mkongwe Rose Ndauka. Akizungumzia umakini wake katika kazi Latipher amesema hivi, “Awali, sikuwa na uzoefu mkubwa katika mambo ya uigizaji, lakini baada ya kukaa ‘camp’ kwa siku kadhaa na kupata mafunzo ya kutosha kutoka kwa wasanii wakongwe nilijikuta nikiingiwa na ujasiri, papo hapo nilianza kujituma na kufanya mazoezi bila kuchoka, nafurahi kuona nilichokipigania kimefanikiwa, nitaendelea kujifunza zaidi ya hapa ili baadae niwe muigizaji bora kabisa wa filamu.” Washiriki wengine aliokutana nao Latipher katika filamu hiyo ni pampja na Mzee Chilo, Hemed Suleiman, Awadh Saleh, Mama Mjata, Timbulo, Peter, Tutti, Miriam na Natalia.

Comments