Dj CHOKA ambae ni DJ na pia msanii kutoka lebo ya B'HITZ MUSIC GROUP.Leo ahsubuhi kwenye mtandao wakijamii wa facebook kupitia account yake alipost maneno ya shukrani kwa mashabiki wake wote na kuelezea kwa kushangazwa kwa upokeaji mkubwa wa nyimbo yake mpya iitwayo "PRESS PLAY" Hivi ndivyo alivyopost"NASEMA NENO MOJA TU ILI ROHO ZENU ZIPONE: Kiukweli sikutarajia na wala sikuamini kwa jinsi mnavyoendelea kunipokea kwa kile ninachokifanya kwenye huu mziki wa nyumbani. Wakati naanza kutoka na PAMOJA WE CAN haikuwa hivi na ndio maana hata natoa hii PRESS PLAY nilichukulia kawaida tu lakini ikawa NDIVYO SIVYO. Nimepata hongera nyingi za kuwa video ya PRESS PLAY ni nzuri sanaaaa. Ila naendelea kutambua kuwa huwezi kufanya kitu peke yako na kikawa kizuri bila kuwa na backup yako nyuma, thanks so much my team BHITZ MUSIC GROUP TANZANIA na bila kuwasahau nyie watanzania kwa sababu wazungu wanasema I HAVE NOTHING WITHOUT YOU. "
Comments
Post a Comment