Wataalam wa mabomu kutoka JWTZ wasema kitu kisichofahamika kilichhoanguka tangu juzi usiku kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani kagera kuwa kitu hicho sio bomu.


Wataalam wa mabomu kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ wamefika katika eneo la Ruganzo wilayani Ngara ambako kitu kisichofahamika kimeanguka tangu juzi usiku na kubaini kuwa kitu hicho sio Bomu.



Mnadhimu mkuu wa mafunzo na utendaji kivita kutoka Briged ya Faru Tabora Kanal Simon Hongoa amesema kuwa kitu hicho kilichoibua hofu kwa wakazi wa eneo hilo na wilaya ya Ngara kwa ujumla sio Bomu bali ni kipande cha Satellite kilichoanguka kutoka  angani.
Aidha wamekichukua kipande hicho cha Satellite na kukihifadhi katika kambi ya jeshi la Wananchi iliyopo eneo la K-9 wilayani  Ngara mkoani Kagera.
Awali kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw Philip Kalangi aliiambia radio kwizera kuwa askari waliofika eneo hilo hapo jana walishindwa kukitambua kitu hicho na kutoa taarifa makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar Es Salaam.
Kipande hicho cha Satellite chenye urefu wa zaidi ya sentimeta 50, kikiwa na umbo la yai pamoja na nyuzinyuzi kilianguka usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo.                Credit to Mwana wa Makonda

Comments