Nyota wa kizazi kipya anayejulikana kwa jina la Lameck Ditto kutoka hapa bongo land Tanzania amechanguliwa katika kuwania tuzo za Radio France International Discoveries ambazo zitakuwa zinatolewa nchini France.katika tuzo hizi wasanii kumi kutoka Africa wamechanguliwa katika kuwania tuzo hizi na Ditto naye ni moja kati ya wasanii ambao wametajwa katika list ya wasanii ambao watashiriki katika kuwania tuzo za Radio France Intenational Discoveries.Kama mshindi akipatikana katika tuzo hizo za Radio France International basi atajipatia Euro elfu kumi na mkataba wa kufanya show live katika nchi 18 Duniani.Kwa hiyo tuna mtakia ushindi katika tuzo hizi za Radio France International
Bonyeza hapa chini kuingia kwenye site ya kumpigia kura
Comments
Post a Comment